Saturday, 8 November 2014

Maafisa wa China watuhumiwa kununuwa pembe za ndovu Tanzania Ununuzi wa pembe hizo ulifanya bei yake kupanda maradufu na kufikia dola za kimarekani 700 kwa kilo moja. Wanadiplomasia wa China, maafisa wa kijeshi na wafanya biashara wa China siku za nyuma walitumia ziara kama hizo kununua shehena kubwa ya pembe za ndovu Tanzania • Ripoti mpya iliyotolewa Alhamis inaeleza kwamba ujumbe wa rais wa China Xi Jinping ulinunua maelfu ya kilo za pembe haramu za ndovu katika ziara yao mwaka 2013 nchini Tanzania. Shtuma hizo zilitolewa katika ripoti ya taasisi inayofuatilia maswala ya Mazingira “Environmental Investigation Agency” kwamba mahitaji ya Wachina kwa pembe haramu za ndovu yanatishia idadi ya Tembo wa Tanzania. Taasisi hiyo imesema ujumbe wa China uliitumia ziara ya Machi mwaka 2013 kutoa kwa magendo pembe za ndovu nje ya nchi kwa kutumia vifurushi vya kidiplomasia kwenye ndege ya rais Xi Jingping. Ripoti ya taasisi hiyo yenye makao yake Uingereza, ilielezea wafanya biashara ya magendo ya pembe za ndovu jijini Dar es salaam na kusema kuwa ununuzi wa pembe hizo ulifanya bei yake kupanda maradufu. Inasema kilo moja ya pembe za ndovu iligharimu dola za kimarekani 700. Pia inasema wanadiplomasia wa China, maafisa wa kijeshi, pamoja na wafanya biashara wa China siku za nyuma walitumia ziara kama hizo kununua shehena kubwa ya pembe za ndovu kennedyrutta



Ununuzi wa pembe hizo ulifanya bei yake kupanda maradufu na kufikia dola za kimarekani 700 kwa kilo moja. Wanadiplomasia wa China, maafisa wa kijeshi na wafanya biashara wa China siku za nyuma walitumia ziara kama hizo kununua shehena kubwa ya pembe za ndovu Tanzania
Ripoti mpya iliyotolewa Alhamis inaeleza kwamba ujumbe wa rais wa China Xi Jinping ulinunua maelfu ya kilo za pembe haramu za ndovu katika ziara yao mwaka 2013 nchini Tanzania.
Ndovu wa Afrika Mashariki
 Shtuma hizo zilitolewa katika ripoti ya taasisi inayofuatilia maswala ya  Mazingira “Environmental

Jumuia ya wafanyakazi wa Afrika Kusini, COSATU, imekitoa katika jumuia chama cha wachimba migodi, NUMSA - chama kikubwa kabisa na chenye malalamiko mengi ya kisiasa katika jumuia hiyo. COSATU imchukua hatua hiyo baada ya NUMSA kulalamika dhidi ya Rais Jacob Zuma, na kukataa kuunga mkono chama tawala cha ANC katika uchaguzi wa awali mwaka huu. NUMSA ilimshutumu Rais Zuma kwamba haungi mkono tena masilahi ya wafanyakazi na kusema kuwa itaanzisha vuguvugu jipya la kishosalisti. Kiongozi wa NUMSA, Irvin Jim, alisema kuwa COSATU - ambayo zamani ikiwatikisa mabosi wakati wa utawala wa ubaguzi wa rangi - sasa imepooza.



Jumuia ya wafanyakazi wa Afrika Kusini, COSATU,imekitoa katika jumuia chama cha wachimba migodi, NUMSA - chama kikubwa kabisa na chenye malalamiko mengi ya kisiasa katika jumuia hiyo.

Tuesday, 4 November 2014

Tiba ya Ebola


Hakuna tibamaalumu ya homa ya Ebola. Lakini ikiwa watu wanapata huduma bora kutokakwa madaktarina wauguzi, wengi wao huishi. Huduma bora kwao inaweza kuwa kwa ugiligili au damu zinazotolewa kwa vena za watu. Inaweza kuwa dawa za kufanya shinikizo la damu na mzunguko wa damu vifanye kazi vizuri.
Ebola huhesabiwa kati ya magonjwa ya mlipuko.
Wagonjwa wa Ebola hutenganishwa na wagonjwa wengine ili wasipate kuwaambukiza. Hii ina maana kwamba watu wengine wasije wakagusa ugiligili na damu yao. Basi watu wengine hawawezi kupata virusi hivi kwa sababu tayari hatua ya kuwatenganisha imeshapita.
Pale mlipuko unapotokea, watu wengi huja na kujaribu kusaidia kuzuia. Shirika la Afya Duniani ni moja kati ya makundi muhimu sana kwa jitihada zake za kujaribu kuzuia mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.

wamarekani-wapiga-kura-uchaguzi-wa-kati-kati-ya-awamu




Wapiga kura kote Marekani wameanza kupiga kura katika uchaguzi wa kati kati ya awamu ambao utaamua kama wa-Democrat au wa-Republican wanadhibiti baraza la seneti katika muda wa miaka miwili uliobaki madarakani kwa Rais Barack Obama.

ManCity yaichapa Manchester United 1-0



Manchester City imeendeleza ubabe wake dhidi ya majirani zao Manchester United kwa kuwachapa goli 1-0 katika mchezo mkali uliofanyika katika uwanja wa Etihad, Jumapili.
Sergio Aguero aliipatia timu yake goli hilo katika dakika ya 63 ya mchezo.
Goli hilo la kumi kwa Aguero katika msimu huu wa ligi kuu ya England liliivunja Manchester United iliyokuwa na ngome iliyosambaratika baada ya Chris Smalling kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika kipindi cha kwanza cha mchezo na Marcos Rojo kutolewa nje katika machela baada ya mapumziko kutokana na kuumia bega.