Mhcezaji wa Manchester CitySergio Aguero akishangilia goli katika ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Manchester
United
Sergio Aguero aliipatia timu yake goli hilo
katika dakika ya 63 ya mchezo.Goli hilo la kumi kwa Aguero katika msimu huu wa ligi kuu ya England liliivunja Manchester United iliyokuwa na ngome iliyosambaratika baada ya Chris Smalling kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika kipindi cha kwanza cha mchezo na Marcos Rojo kutolewa nje katika machela baada ya mapumziko kutokana na kuumia bega.
Manchester City walikuwa mabingwa watetezi wa kombe hilo.
Mchezo kati ya Manchester City na Manchester United ulikuwa mpambano mkali, ukiwa wa kwanza kwa meneja mpya wa Manchester United, Louis van Gaal, akishuhudia ngome ya timu yake ikiyumba na nguvu ya safu ya ushambuliaji ya kina Angel Di Maria, Robin van Persie na Wayne Rooney ikishindwa kupeleka michomo iliyotarajiwa katika lango la Manchester City.
Kwa matokeo hayo Chelsea bado inashikilia usukani wa ligi kuu ya England ikiwa na pointi 26, pointi sita juu ya Manchester City na pointi nne juu ya Southampton inayoshikilia nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo.
Manchester United iko katika nafasi ya kumi baada ya michezo kumi ikiwa na pointi 13, huku Burnely ikiwa katika nafasi ya ishirini na ya mwisho katika ligi kuu hiyo, kwa kujikusanyia pointi nne tu katika michezo yake kumi iliyokwishachezan .NA KENNEDYRUTTA WA ARUSHA
No comments:
Post a Comment