Tuesday, 4 November 2014

Tiba ya Ebola


Hakuna tibamaalumu ya homa ya Ebola. Lakini ikiwa watu wanapata huduma bora kutokakwa madaktarina wauguzi, wengi wao huishi. Huduma bora kwao inaweza kuwa kwa ugiligili au damu zinazotolewa kwa vena za watu. Inaweza kuwa dawa za kufanya shinikizo la damu na mzunguko wa damu vifanye kazi vizuri.
Ebola huhesabiwa kati ya magonjwa ya mlipuko.
Wagonjwa wa Ebola hutenganishwa na wagonjwa wengine ili wasipate kuwaambukiza. Hii ina maana kwamba watu wengine wasije wakagusa ugiligili na damu yao. Basi watu wengine hawawezi kupata virusi hivi kwa sababu tayari hatua ya kuwatenganisha imeshapita.
Pale mlipuko unapotokea, watu wengi huja na kujaribu kusaidia kuzuia. Shirika la Afya Duniani ni moja kati ya makundi muhimu sana kwa jitihada zake za kujaribu kuzuia mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.

Ebola ni virusi vya homa ya hemoraji (yaani "kumwaga damu sana"). Huo ugonjwa wa damu kutoganda unaua sana. Kati ya watu 10 waliopata virusi vya Ebola, basi wastani kati ya watano na tisa h Dalili za Ebola

Pale watu wanapopata Ebola, dalili zake za kwanza ni kuonekana kama magonjwa mengine. Watu wanapata homa, kujisikia kuchoka, maumivu ya kichwa, maumivu ya tumbo, maumivu katika viungo vyao, na maumivu kooni. Kwa dalili hizo, watu hufikiria kwamba wana magonjwa mengine kama vile malaria au homa ya matumbo.
Baadaye, hali inakuwa mbaya zaidi, hadi kufikia hali ya kumwaga damu kwa kiasi kikubwa sana. Wanapata mshtuko: shinikizo la damu kuwa chini, mapigo ya moyo kwenda kasi, na mzunguko wa damu kuwa hafifu mwilini. Hii inasababisha viungo vya mwili kuuma sana. Viungo vya mwili vinaacha kufanya kazi.

No comments:

Post a Comment