Siku kama ya leo miaka 36
iliyopita, wanajeshi wa utawala wa kidikteta wa Pahlavi walisambaratisha
maandamano makubwa ya wananchi wa mji wa Tehran nchini Iran. Wananchi Waislamu
wakazi wa Tehran siku hiyo walianza kuandamana tangu asubuhi, hayo yakiwa
maandamano ya siku kadhaa mfululizo kuwahi kufanywa na wakazi wa mji wa Tehran
dhidi ya utawala wa kibaraka wa Pahlavi. Wakati huo, utawala wa kijeshi ulikuwa
umetangazwa katika mji wa Tehran, lakini wananchi Waislamu bila ya kuzingatia
hali hiyo, wakamiminika mitaani wakipiga nara dhidi ya utawala wa Shah. Wakati
huo huo walinzi maalumu wa Shah walifanya mashambulizi na katika muda mfupi
wakawaua shahidi wananchi zaidi ya elfu nne wa Tehran waliokuwa wakipigania
haki zao.
Miaka 60 iliyopita katika siku kama
ya leo, mkataba wa SEATO wa makubaliano ya kiulinzi ya Asia ya Kusini-Mashariki
ulisainiwa katika mji mkuu wa Ufilipino, Manila. Serikali za Marekani,
Uingereza, Australia, Pakistan, Thailand, Ufaransa, New Zealand na Ufilipino
ndizo zilizosaini mkataba huo. Nchi hizo zilikubaliana kusaidiana iwapo
zingeshambuliwa na nchi nyingine au kukabiliwa na uasi wa ndani.
Miaka 91 na katika siku kama ya leo,
sawa na tarehe 12 Dhil Qaada mwaka 1344 Hijiria, alifariki dunia Adib
Neishabur, mshairi maarufu wa Iran. Neishabur alizaliwa mwaka 1281 Hijiria
katika mji wa Neishabur kaskazini mwa Iran, na utotoni mwake alipatwa na maradhi
ya tete kuwanga yaliyompelekea kuwa kipofu. Lakini suala hilo halikumrudisha
nyuma na kwa jitihada nyingi alijishughulisha kutafuta elimu na kuwa mahiri
katika fasihi ya Kiarabu na Kifarsi. Katika maisha yake, Neishabur
alijishughulisha na utunzi wa mashairi na kuandika vitabu vingi katika uwanja
huo.
Na miaka 73 iliyopita muwafaka
na leo, wanajeshi wa Ujerumani ya Kinazi waliuzingira mji wa Leningrad, Saint
Petersburg ya sasa. Hata hivyo mji huo haukutekwa na jeshi la Kinazi, licha ya
utabiri wa Adolf Hitler na makamanda wake. Wakazi wa Leningrad waliendeleza
mapambano ya ukombozi hadi Januari mwaka 1944, wakati walipofanikiwa kujiondoa
katika mzingiro wa wanajeshi wa Ujerumani
No comments:
Post a Comment