·
Kwa
mara nyingine tena chama cha 'Mrengo wa Kitaifa kwa ajili ya Marekebisho'
nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kimesisitiza kuwa hatua ya kuifanyia
marekebisho ya katiba ya nchi hiyo ina maana ya kuibua machafuko nchini.
Viongozi wa chama hicho kwa kushirikiana na vyama vingine vya upinzani nchini
Kongo wamelaani njama zozote za kutaka kutekeleza jambo hilo. Kabla ya hapo
chama kilichoungana na chama tawala cha 'Wananchi kwa ajili ya Marekebisho na
Demokrasia' kilitangaza azma ya kuifanyia marekebisho katiba ya Kongo. Kwa
mujibu wa habari, marekebisho hayo yatahusu kipengee cha 220 ambapo ikiwa hatua
hiyo itaungwa mkono na wananchi katika kura ya maoni, basi itatoa fursa kwa
Rais Joseph Kabila kugombea kwa mara ya tatu katika uchaguzi mkuu ujao. Rais
Kabila ambaye alichukua uongozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya
kuuawa baba yake Laurent-Désiré Kabila hapo mwezi Juni mwaka 2001, alishinda
katika uchaguzi wa mwaka 2006 na 2011.
mjusi blogspot.com Katika safari yake nchini Marekani mwezi
Agosti mwaka huu na katika kikao na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, John
Kerry, Rais Kabila hakuweza kutoa jibu lililo wazi alipoulizwa na Kerry kuhusu
azma yake ya kuifanyia marekebisho katiba. Tangu aliposhika madaraka ya nchi,
Joseph Kabila amekuwa muitifaki mkubwa wa Marekani katika eneo la Maziwa Makuu
ya Afrika. Kwa mujibu wa weledi wa mambo, kuanguka dikteta Mobutu Sese Seko
hapo mwaka 1997, kulikuwa ni pigo kubwa kwa Ufaransa, na ushindi muhimu kwa
Marekani. Hivi sasa John Kerry, amemtaka Rais Kabila achunge kanuni za
demokrasia nchini mwake. Pamoja na yote hayo rais huyo kijana wa Kongo DRC
hakuwa tayari kutoa jibu la wazi kwa Kerry. Suala hilo linaelezwa kuwa
linatokana na Kabila kutaka kuwa na uhuru wa maamuzi na kupinga aina yoyote ya
uingiliaji wa kigeni katika mambo ya ndani ya nchi yake. Itakumbukwa kuwa,
mabadiliko ya Katiba ya Februari mwaka 2012 nchini Kongo DRC yalipelekea pia
kutokea upinzani mkubwa wa vyama vya upinzani. Kwa mujibu wa vyama hivyo,
mabadiliko hayo yalikuwa ni kwa maslahi ya chama tawala. Hivi sasa vyama vya
upinzani na wakosoaji wa serikali ambao kwa pamoja waliunda muungano kwa ajili
ya kukabiliana na mabadiliko ya katiba nchini humo, wamewataka wananchi
kumiminika mabarabarani na kufanya maandamano makubwa hapo tarehe 13 mwezi huu.
Weledi wa mambo wanayataja maandamano hayo tarajiwa kwamba yanaweza kuwa mwanzo
wa upinzani wa wananchi unaoungwa mkono pia na shakhsia wakubwa wa
kisiasa nchini humo. Miongoni mwa shakhsia hao ni pamoja na mzee Etienne Tshisekedi
ambaye ni mpinzani nambari moja wa Rais Kabila na mwenye wafuasi wengi nchini
Kongo. Suala muhimu la kufaa kuzingatiwa ni kwamba, baada ya harakati za uasi
wa wananchi zilizojiri katika nchi mbalimbali, harakati hizo zinaweza
kuwaathiri pia Wakongomani na hivyo kuanzisha wimbi kubwa la uasi dhidi ya Rais
Joseph Kabila wa nchi hiyo
No comments:
Post a Comment