Monday, 8 September 2014

Alshabaab wamteua kiongozi mpya




Kiongozi huyo mpya ni Ahmad Umar ambaye hajulikani sana. Mmoja wa makomandawa Al Shabaab Abu Mohammed, alisema uamuzi wa kumteua kiongozi huyo ulifikiwa bila pingamizi.
  • http://kiswahili.irib.ir/media/k2/items/cache/01a5bf934eaed0c12b6cbc6810e1ab64_XL.jpgSomalia
Kundi hilo lilitoa tangazo lao kupitia kwenye mtandao wakiahidi kulipiza kisasi mauaji ya Ahmed Godane.
Maafisa wakuu nchini Somalia awali walitoa taarifa ya tahadhari wakionya dhidi ya mashambulizi ya kulipiza kisasi kutoka kwa kundi hilo.
Al Shabaab wameahidi kulipiza kisasi mauaji ya Ahmed Godane
Tahadhari hiyo ilitolewa huku Marekani ikithibitisha kifo cha Godane kilichotokea kufutia shambulizi la angani lililofanywa na wanajeshi wa Marekani Jumatatu usiku wiki jana.
Msemaji wa Alshabaab amesema kuwa wapiganaji wengine wawili wa kundi hilo pia walifariki katika shambulizi hilo ,yapata kilomita 170 Kusini ya mji mkuu wa Mogadishu .
Katika taarifa yao,kundi hilo lilionya :"kulipiza kisasi mauaji ya kiongozi wetu ni jukumu letu ambalo hatutawahi kukoksa kutekeleza licha ya muda.''
Kwa ruhusa ya Mwenyezi Mungu , bila shaka mtaonjeshwa makali ya adhabu ya milichokifanya.
Tangazo la kiongozi huyo mpya llitolewa dakika chahe tu baada ya kundi hilo kuthibitisha kifo cha Godane.
Mapema JUmapili, waziri wa usalama wa ndani, alisema kuwa seriklali ilipokea taarifa za kundi hilo kupanga kushambulia vituo vya afya, el;imu na taasisi zengine za serikali nchini humo.

No comments:

Post a Comment