Sunday, 14 September 2014

Je, Afrika Kusini ni ‘Nchi Iliyokwama'? Ndivyo Alan Dershorwitz Anavyofikiri

Waafrika Kusini wamekuja juu kuitetea nchi yao baada ya mwanasheria wa Kimarekani na mchambuzi wa duru za kisiasa Alan Dershorwitz kuiita Afrika Kusini kuwa ni “nchi iliyokwama “ wakati akijadili mashitaka ya mauaji ya  Oscar Pistorius  kwenye kipindi cha Piers Morgan kwenye chaneli ya habari ya CNN.
Mwanariadha huyo wa Afrika Kusini asiye na miguu yote miwili  alimpiga risasi na kumwuua rafiki yake wa kike Reeva Steenkamp mnamo Februari 14, 2013; bingwa huyo wa mashindano ya Olimpiki anadai kuwa alidhani anamwuua mtu mhalifu aliyevamia nyumba yake.
American lawyer and political commentator Alan Dershowitz. Photo released under Creative Commons by Flickr user The Huntington.
Mwanasheria wa Marekani na mchambuzi wa mambo ya kisiasa Alan Dershowitz. Picha imetolewa kwa haki miliki ya Creative Commons na mtumiaji wa Flickr aitwaye The Huntington.
Dershorwitz alitoa maoni kwenye mahojiano , “Nimekaa kidogo nchini Afrika Kusini hivi karibuni, na watu hawataki kusikia hili, lakini Afrika Kusini ni nchi iliyokwama.”
Mtazame Dershowitz akitoa matamshi hayo hapa chini:
Muda mfupi baadae, wataalamu wa Uchumi nchini Afrika Kusini walijitokeza kukanusha matamashi hayo, wakisema kuwa nchi ya Afrika Kusini haina vigezo vyovyote vya kuitwa “taifa lililokwama kiuchumi” kama vile ghasia zilizoenea za wenyewe kwa wenyewe, kutokufanya kazi kwa asasi za kiraia, kutokuwepo kwa mhimili wa mahakama unaojitegemea na kutokuwepo kwa ulinzi wa mali za watu.
Waafrika Kusini waliingia kwneye mtandao wa Twita kuonyesha hasira zao na kukana kabisa madai hayo

No comments:

Post a Comment