Katika Hatua nyingine, nchi ya Cote d'Ivoire imetangaza hali ya tahadhari na kupiga marufuku usafiri wa ndege kutoka nchi zilizoathirika na virusi vya Ebola pamoja na makampuni yote ya kusafirisha abiria kuelekea mjini Abidjan.
Nchini Sierra Leone, raia wa China nane wamewekwa karantini baada ya kuhudumia wagonjwa wa Ebola wakati Nigeria ikithibitisha ambukizi mpya siku ya Jumatatu na nchi ya Rwanda ikisubiria matokeo ya vipimo vinavyofanyika kuhusu mjerumani mmoja ambaye kwa siku kadhaa amekuwa Liberia na kuanza kuonyesha dalili za homa ya Ebola.
Hayo yakijiri, Japan imeamua kuwaondoa maafisa wake 24 waliokua wakifanya kazi nchini Guinea, Liberia na Sierra Leone kufutia mlipuko huo wa Homa ya Ebola, ambayo inaendela kuyakumba mataifa ya Afrika Magharibi, na kusababisha vifo vya watu 1013, kulingana na takwimu zilizotolewa na WHO.
“Zowezi la kuwaondoa maafisa hao litatamatika mnamo ziku za hivi karibuni”, msemaji wa taasisi ya Japan inayohusika na ushirikiano wa kimataifa (JICA), Yuho Hayakawa amesema.
Maafisa hao wa Japan wamekua wakifanya kazi katika sekta ya kilimo, afya na ukandarasi
No comments:
Post a Comment