Wednesday, 26 August 2015

Umoja usio rasmi wa vyama vinne vya upinzani nchini Tanzania unajulikana kwa jina la Katiba ya Wananchi (UKAWA),



 baada ya kusubiri kwa muda hatimaye umemtangaza Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa kuwa mgombea wake wa urais.
Lowassa anagombea kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), huku vyama vingine vitatu vikimuunga mkono. Hii inatokana na sheria za Tanzania ambayo haitambui umoja wa vyama.
Kabla ya kujiengua chama Tawala chama cha Mapinduzi CCM, Edward Lowassa amekuwa mwanachama wa CCM kwa muda wa miaka 38, ambapo alijiunga na chama hicho mara tu baada ya kumaliza elimu yake ya chuo kikuu mwaka 1977.

Thursday, 16 July 2015

Tuzo ya Grammy kwa Albamu bora zaidi


Kutoka mjusi, blog elezo huru
Tuzo ya Grammy kwa Albamu bora zaidi
Tuzo kwa albamu bora kwa rapping
Nchi United States
Yaliyowasilishwa na National Academy ya kurekodi Sanaa na Sayansi
Kwanza tuzo 1996
Mwisho tuzo 2015
Tovuti rasmi grammy.com
Tuzo ya Grammy kwa ajili ya Albamu bora zaidi ni tuzo iliyotolewa kwa kurekodi wasanii kwa ajili ya albamu bora kwa rapping katika tuzo ya Grammy, sherehe ambayo ilianzishwa mwaka 1958 na awali aitwaye gramafoni Awards. [1] Heshima katika makundi kadhaa ni iliyotolewa katika sherehe kila mwaka na Chuo cha Taifa cha Recording Sanaa na Sayansi ya United States na "heshima mafanikio kisanii, ustadi wa kiufundi na ubora wa jumla katika sekta ya kurekodi, bila kujali mauzo ya albamu au nafasi chati". [2]

Mwaka 1995, Chuo alitangaza kuongeza ya tuzo jamii Albamu bora zaidi. [3] tuzo ya kwanza iliwasilishwa kwa kundi Naughty by Nature kwa 38 Tuzo za Grammy mwaka uliofuata. Kwa mujibu wa jamii maelezo mwongozo kwa ajili ya 52 Tuzo za Grammy, tuzo zimetolewa kwa ajili ya "Albamu zenye angalau 51% kucheza wakati wa nyimbo na wapya kumbukumbu rapped maonyesho". [4] Tuzo wapokeaji mara nyingi ni pamoja wazalishaji, wahandisi, na / au mixers kuhusishwa na kazi ameshinda kwa kuongeza wasanii kurekodi. [5]

                                                         Death row recordni kampuni yakurekodi ya Kaskazini ilianzishwa mwaka 1991 na Harry OTracy "DOC"Lynn Curry, Andre "Dr. Dre" Young, Marion "Suge" Knight Jr.na West Coast hip hop wasanii, ikiwa ni pamoja na Snoop Dogg, Tupac Shakur, Outlawz, Mama wa Rage, MC Hammer, Young Soldierz, Sam Sneed, LBC wafanyakazi, RBX, Michel'le, Jewell, Danny Boy, DJ Quik, OFTB, Nate Dogg na rap kundi Tha Dogg Pound yenye wasanii Kurupt, Daz, Soopafly, na wengine wengi. Wengi kama sio wote alitoka studio baada ya mauaji ya Tupac Shakur mwaka 1996. kampuni filed kwa kufilisika mwaka 2006 na mnamo Januari 15, 2009, ilikuwa mnada kwa kampuni ya burudani ya maendeleo WIDEawake Entertainment Group, Inc ajili $ 18,000,000.

Saturday, 27 December 2014

Jumatano, 24 Disemba 2014 07:10 Uislamu na Mtindo wa Maisha(48) ukubwa wa hati ukubwa wa hati kuzisha hati Kichapishi Add new comment Uislamu na Mtindo wa Maisha(48) Hamjambo na karibuni kuwa nasi tena katika sehemu nyingine ya makala ya Uislamu na Mtindo wa Maisha. Makala yetu leo inaendelea kuzungumzia misingi ya jinsi ya kuamiliana na watoto kwa mujibu wa mtindo wa maisha wa Kiislamu. Wataalamu wa elimu nafsi wanasema kuwa, moja kati ya mahitaji muhimu ya mwanadamu baada ya mahitaji ya kimsingi ya kiumbe huyo kama maji na chakula, ni haja ya kupendwa. Kupendwa kuna umuhimu mkubwa sana kwa kadiri kwamba iwapo haja hiyo haitakidhiwa, basi suala hilo linaweza kuwa na taathira mbaya katika maisha ya mwanadamu. Haja ya kupendwa huwa kubwa zaidi katika nafsi ya mtoto na kukidhiwa kwake kwa njia sahihi ni nguzo na msingi muhimu wa malezi bora. Kumpenda mtoto humzidishia utulivu wa kiroho na kinafsi, hali ya kujiamini na kuwategemea na kuwaamini zaidi wazazi wake. Katika upande wa pili, kutoshibishwa haja hiyo ya kupendwa katika nafsi ya mtoto humuondolea utulivu na usalama wa kiroho na kinafsi, kumfanya asijiamini yeye na watu wengine, kujihisi hakiri na duni na pengine kumsababishia matatizo ya kimwili na kinafsi, utovu wa maadili na kutumbukia katika ufuska. Familia yenye mlingano katika mtindo wa maisha wa Kiislamu ni familia ambayo wanachama wake wanasifika kwa kuwa na uhusiano unaotawaliwa na upendo na mahaba baina yao. Viongozi wa dini yetu tukufu ya Uislamu pia wamefanya jitihada kubwa za kuwahimiza Waislamu kujenga uhusiano wao wa kifamilia kwa msingi wa upendo na mahaba baina yao. Imam Swadiq (as) ameeleza kuwa miongoni mwa mambo yanayoteremsha rehma za Mwenyezi Mungu kwa mja wake ni kumpenda sana mtoto. Anasema: “Mwenyezi Mungu humrehemu na kumteremshia rehma mtu anayempenda sana mwanaye”. Tumesema kuwa upendo na mahaba vimehimizwa sana kati ya watu wa familia. Hata hivyo tunasisitiza kuwa, uadilifu na insafu inapaswa kuzingatiwa na kuchungwa katika namna ya kuamiliana na watu ndani ya familia. Kwa mfano mahaba na upendo wa wazazi wawili kwa mtoto mmoja katika familia unapovuka mipaka ya uadilifu na insafu yumkini ukawa na taathira nyingi mbaya kwa watoto kama husuda, kujiona duni, kukata uhusiano na wazazi na kuwa na vinyongo kwa watoto wengine. Vilevile kuamiliana kibaguzi na watoto yumkini kukahatarisha msingi wa familia katika siku za usoni. Kwa kuzingatia hayo Mtume Muhammad (saw) alipomuona bwana mmoja akimbusu mmoja kati ya watoto wake na kumuacha mwingine alilalamika na kumwambia: Kwa nini huamiliani nao kwa usawa? Mtukufu Mtume pia amewaambia Waislamu kwamba: “Amilianeni na watoto wenu kwa uadilifu kama mnavyopenda kufanyiwa wema na uadilifu”. Taasisi ya familia inapaswa kuwa anga iliyojaa upendo na mahaba. Anga ya utulivu, upendo na mahaba ndani ya familia na mwenendo mzuri wa wazazi kwa watoto huwa na shifaa na tiba ya kinafsi kwa watoto na huwatayarishia mazingira mazuri ya kustawi katika nyanya mbalimbali. Aina ya uhusiano wa wazazi na watoto wao ndani ya familia huwa msingi wa mahusiano yao ya baadaye na watu wengine. Imam Muhammad Ghazali anasema katika kitabu cha Kemia ya Saada kwamba: Elewa kwamba, mtoto ni amana katika mikono ya baba na mama, na nafsi yake safi ni mithili ya johari yenye thamani kubwa. Ni kama nta inayokubali umbo na sura tofauti, na mithili ya ardhi safi ambayo kila kinachopandwa humo kinaota na kumea. Kama utapanda mbegu ya kheri katika ardhi hiyo itamfikisha katika saada na ufanisi wa dunia na akhera, na baba, mama na mwalimu watashirikiana na mtoto huyo katika thawabu zake; na kinyume chake, mtoto huyo hukumbwa na masaibu na wazazi na mwalimu hushirikiana naye pia katika hayo”, mwisho wa kunukuu. Miongoni mwa mambo muhimu kuhusu suala la kuwapenda watoto ni kwamba tusitosheke na kuwapenda katika nyoyo zetu tu, kwani upendo na mahaba huwa na taathira pale vinapodhihirishwa na kumuonesha mtoto kwamba anapendwa. Imam Ali bin Abi Twalib (as) alidhihirisha upendo na mahaba yake kwa mwanaye, Hassan bin Ali (as), katika barua aliyomwandikia akisema: “Nakutambua kuwa wewe ni sehemu yangu mimi bali wewe ni mimi mzima kwa kadiri kwamba kinachokusibu wewe huwa kama kimenisibu mimi na kana kwamba mauti yakikufika wewe ni sawa na kunifika mimi. Hivyo basi mambo yako yanaishughulisha nafsi yangu kama ninavyoshughulishwa na yangu mwenyewe na kwa msingi huo nakuandikia barua hii ili nipate kudhihirisha upendo na mahaba yangu kwako..”. Kuonesha na kudhihirisha upendo na mahaba ni miongoni mwa misingi muhimu ya uhusiano wa wazazi na watoto wao. Hali zetu za kiroho hutusaidia sana katika kuchukua maamuzi na kutoa hukumu na maoni. Vilevile wazazi wanaodhihirisha upendo na mahaba kwa watoto huzidisha hali ya upendo na mahaba baina yao wenyewe na matokeo yake ni kuimarisha uhusiano wa watoto na wazazi wao. Wataalamu wa elimu nafsi wanasema kuwa, utafiti uliofanywa kuhusu upotofu na utovu wa maadili wa watoto umebaini kuwa, kuna sababu nyingi za jambo hilo ikiwa ni pamoja na ukosefu wa mahusiano mazuri na yenye upendo na mahaba ya wazazi kwa watoto wao. Mafundisho ya Uislamu yamehimiza sana juu ya udharura wa kudhihirisha hisia za ndani ya nafsi. Mazungumzo yaliyojaa hisi za upendo na mahaba kwa watoto, kumtazama mtoto kwa jicho na upendo, mahusiano yasiyo ya maneno na watoto kama kumbusu, kumpakata na kumpapasa kichwani kulingana na umri wa mtoto, ni miongoni mwa vielelezo vya kudhihirisha hisi za upendo na mahaba kwa mtoto wako. Mtume Muhammad (saw) anasema kuhusu suala hilo kwamba: Mtu anayembusu mtoto wake, Mwenyezi Mungu humwandikia amali njema, na mtu anayemfurahisha mtoto wake M, Mungu atamfurahisha Siku ya Kiyama". (Usulul Kafi: 6-49) Miongoni mwa misingi muhimu ya uhusiano wa wazazi na watoto ni kuwaruhusu kueleza mitazamo, hisia na maamuzi yao kwa uhuru. Suala hilo lina maana kwamba, tutakuwa tumempa mtoto haki ya kukosea isipokuwa katika masuala ambayo makosa kama hayo ni hatari kwake yeye na kwa watu wengine. Kabla ya jambo lolote, wazazi wawili wanapaswa kuwa wasikilizaji wazuri ili waweze kuwa wasaidizi na waelekezaji bora wa watoto wao. Watoto wana haja ya kuhisi kwamba, wanapendwa na kukubaliwa na wazazi wao, japo wakati mwingine wanakosea na kutumbukia katika makosa. Kabla ya watoto kuwa tayari kusikiliza maneno ya mzazi, wanapaswa kwanza kuhisi kwamba maneno yao yanasikilizwa na wazazi, na kabla ya kueleza fikra, hisia na matakwa yao, kwanza wanapaswa kufikia natija kwamba wazazi wao wanawaelewa na kuwathamini. Dakta Ghulam Ali Afruz ambaye ni mtaalamu wa saikolojia wa Iran anasema: Mtoto ana haki ya kepata upendo, utanashati na hisia za kukubalika ndani ya taasisi ya familia. Anaendelea kwa kusema: Mtume Muhammad (saw) amesema, katika miaka saba ya kwanza ya uhai wake, mtoto huwa mwenye kupendwa, na kipindi cha miaka saba ya pili huwa tayari kufundishwa na katika saba la tatu huwa mshauri. Kipindi cha miaka saba ya awali ndicho kipindi cha kuweka misingi imara ya shakhsia ya mtoto. Kwa kawaida watoto hupenda kupitisha kipindi hicho kwa utanashati, upendo na katika anga ya uhusiano wenye vuguvugu na mahaba ya wazazi. Vilevile watoto wana haki ya kuheshimiwa, na hupendelea kuthaminiwa na kuenziwa na watu wengine. Kwa msingi huo, anamalizia Dakta Ghulam Ali, miongoni mwa nyadhifa muhimu na majukumu makubwa ya baba na mama ni kuwakirimu, kuwathamini na kuwaheshimu watoto wao.


Hamjambo na karibuni kuwa nasi tena katika sehemu nyingine ya makala ya Uislamu na Mtindo wa Maisha. Makala yetu leo inaendelea kuzungumzia misingi ya jinsi ya kuamiliana na watoto kwa mujibu wa mtindo wa maisha wa Kiislamu.
Wataalamu wa elimu nafsi wanasema kuwa, moja kati ya mahitaji muhimu ya mwanadamu baada ya mahitaji ya kimsingi ya kiumbe huyo kama maji na chakula, ni haja ya kupendwa. Kupendwa kuna umuhimu mkubwa sana kwa kadiri kwamba iwapo haja hiyo haitakidhiwa, basi suala hilo linaweza kuwa na taathira mbaya katika maisha ya mwanadamu. Haja ya kupendwa huwa kubwa zaidi katika nafsi ya mtoto na kukidhiwa kwake kwa njia sahihi ni nguzo na msingi muhimu wa malezi bora. Kumpenda mtoto humzidishia utulivu wa kiroho na kinafsi, hali ya kujiamini na kuwategemea na kuwaamini zaidi wazazi wake.Jumatano, 24 Disemba 2014 07:10 Uislamu na Mtindo wa Maisha(48) ukubwa wa hati ukubwa wa hati kuzisha hati Kichapishi Add new comment Uislamu na Mtindo wa Maisha(48) Hamjambo na karibuni kuwa nasi tena katika sehemu nyingine ya makala ya Uislamu na Mtindo wa Maisha. Makala yetu leoi

Kiongozi wa Al-Shabaab akamatwa





Kundi la wapiganaji wa Al shabaab
Maafisa nchini Somali wanasema kuwa kiongozi mkuu wa kundi la wapiganaji wa Alshabaab amekamatwa karibu na mji mmoja karibu na mpaka wa Kenya na Somali

Saturday, 8 November 2014

Maafisa wa China watuhumiwa kununuwa pembe za ndovu Tanzania Ununuzi wa pembe hizo ulifanya bei yake kupanda maradufu na kufikia dola za kimarekani 700 kwa kilo moja. Wanadiplomasia wa China, maafisa wa kijeshi na wafanya biashara wa China siku za nyuma walitumia ziara kama hizo kununua shehena kubwa ya pembe za ndovu Tanzania • Ripoti mpya iliyotolewa Alhamis inaeleza kwamba ujumbe wa rais wa China Xi Jinping ulinunua maelfu ya kilo za pembe haramu za ndovu katika ziara yao mwaka 2013 nchini Tanzania. Shtuma hizo zilitolewa katika ripoti ya taasisi inayofuatilia maswala ya Mazingira “Environmental Investigation Agency” kwamba mahitaji ya Wachina kwa pembe haramu za ndovu yanatishia idadi ya Tembo wa Tanzania. Taasisi hiyo imesema ujumbe wa China uliitumia ziara ya Machi mwaka 2013 kutoa kwa magendo pembe za ndovu nje ya nchi kwa kutumia vifurushi vya kidiplomasia kwenye ndege ya rais Xi Jingping. Ripoti ya taasisi hiyo yenye makao yake Uingereza, ilielezea wafanya biashara ya magendo ya pembe za ndovu jijini Dar es salaam na kusema kuwa ununuzi wa pembe hizo ulifanya bei yake kupanda maradufu. Inasema kilo moja ya pembe za ndovu iligharimu dola za kimarekani 700. Pia inasema wanadiplomasia wa China, maafisa wa kijeshi, pamoja na wafanya biashara wa China siku za nyuma walitumia ziara kama hizo kununua shehena kubwa ya pembe za ndovu kennedyrutta



Ununuzi wa pembe hizo ulifanya bei yake kupanda maradufu na kufikia dola za kimarekani 700 kwa kilo moja. Wanadiplomasia wa China, maafisa wa kijeshi na wafanya biashara wa China siku za nyuma walitumia ziara kama hizo kununua shehena kubwa ya pembe za ndovu Tanzania
Ripoti mpya iliyotolewa Alhamis inaeleza kwamba ujumbe wa rais wa China Xi Jinping ulinunua maelfu ya kilo za pembe haramu za ndovu katika ziara yao mwaka 2013 nchini Tanzania.
Ndovu wa Afrika Mashariki
 Shtuma hizo zilitolewa katika ripoti ya taasisi inayofuatilia maswala ya  Mazingira “Environmental

Jumuia ya wafanyakazi wa Afrika Kusini, COSATU, imekitoa katika jumuia chama cha wachimba migodi, NUMSA - chama kikubwa kabisa na chenye malalamiko mengi ya kisiasa katika jumuia hiyo. COSATU imchukua hatua hiyo baada ya NUMSA kulalamika dhidi ya Rais Jacob Zuma, na kukataa kuunga mkono chama tawala cha ANC katika uchaguzi wa awali mwaka huu. NUMSA ilimshutumu Rais Zuma kwamba haungi mkono tena masilahi ya wafanyakazi na kusema kuwa itaanzisha vuguvugu jipya la kishosalisti. Kiongozi wa NUMSA, Irvin Jim, alisema kuwa COSATU - ambayo zamani ikiwatikisa mabosi wakati wa utawala wa ubaguzi wa rangi - sasa imepooza.



Jumuia ya wafanyakazi wa Afrika Kusini, COSATU,imekitoa katika jumuia chama cha wachimba migodi, NUMSA - chama kikubwa kabisa na chenye malalamiko mengi ya kisiasa katika jumuia hiyo.