baada ya kusubiri kwa muda hatimaye umemtangaza Waziri Mkuu wa zamani Edward
Lowassa kuwa mgombea wake wa urais.
Lowassa anagombea kupitia Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), huku vyama vingine vitatu vikimuunga mkono.
Hii inatokana na sheria za Tanzania ambayo haitambui umoja wa vyama.
Kabla ya kujiengua chama Tawala chama
cha Mapinduzi CCM, Edward Lowassa amekuwa mwanachama wa CCM kwa muda wa miaka
38, ambapo alijiunga na chama hicho mara tu baada ya kumaliza elimu yake ya
chuo kikuu mwaka 1977.
Hatua ya mwanasiasa huyo mashuhuri
nchini Tanzania kuamua kujiunga na chama cha upinzani Chadema, ikiwa imebaki
miezi mitatu tu kuelekea uchaguzi mkuu, kumebadilisha kabisa upepo wa kisiasa
nchini Tanzania, na hasa uchaguzi mkuu ujao.
Image caption Wasifu wa Lowassa
Lowassa alikuwa Maziri Mkuu kati ya
mwaka 2005 na 2008 kabla ya kujiuzuLu wadhifa huo kufuatia sakata la kashfa ya
rushwa iliyohusisha kampuni ya kuzalisha umeme ya ki-Marekani Richmond
Development Company LLC ya Houston Texas.
Hata hivyo wakati anatangazawasifu wa lowassa kuhamia kwake Chadema, Lowassa alikanusha katu katu kuhusika kwa namna yoyote na kashfa hiyo na kudai kuwa yeye alifuata tu amri kutoka kwa ‘wakubwa’ walio juu yake.
“Kama kuna mtu yeyote mwenye ushahidi
basi na aende mahakamani ama sivyo anyamaze” alisema Lowassa
Image caption “Kama kuna mtu yeyote
mwenye ushahidi basi na aende mahakamani ama sivyo anyamaze” alisema Lowassa
Kuhama kwake kunamfanya Lowassa kuwa
ndie kiongozi wa kwanza wa ngazi ya juu kabisa wa CCM kukihama chama hicho
tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi nchini Tanzania mnamo mwaka 1992.
Mwanajeshi wa zamani na aliyewahi
kupigana wa vita kati ya Uganda na Tanzania mwaka 1978/79, Lowassa aliiambia
hadhara kwamba akiwa kama mtu mwenye uchungu na nchi yake isingekuwa rahisi
kubaki ndani ya CCM huku akiona chama hicho kimepoteza mwelekeo na sifa ya
kuongoza nchi.
Lowassa amekimbilia upinzani baada jina
lake kukatwa wakati alipoomba kuwa mgombea urais kupitia chama tawala CCM
katika uchaguzi mkuu ujao utakafanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Wakati mchakato wa CCM wa kumtafuta
mgombea wao wa urais ulipoanza, Lowassa ndiye aliyekuwa kinara wa wagombea wote
42. Kila kona aliyozunguka, mikutano yake ya hadhara ilivutia maelfu ya watu
waliomuunga mkono.
Wakati chama cha CCM kilimtaka kila
mgombea apate sahihi za wadhamini 450 lakini Lowassa alipata sahihi za
wadhamini zaidi ya 700,000.
Image caption Wasifu wa Edward Lowassa
Hata hivyo mchujo wa chama ulipofanyika
jina lake lilikatwa mapema kabla hata ya kupelekwa kwenye vikao vya vya juu vya
chama hicho. Ambapo baadae Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli ndiye
aliyeibuka kidedea na kuwa mgombea kupitia chama tawala CCM.
Lowassa ameushutumu mchakato CCM wa
kutafuta mgombea urais akiuita kuwa ulijaa chuki na mizengwe dhidi yake, hali
ambayo aliifananisha na ‘ubakaji wa demokrasia’
“Nitakuwa mnafki nikisema bado nina
imani na CCM. CCM niliyoiona Dodoma si CCM niliyokulia”, alisema, na kuongeza
“kama Watanzania hawapati maendeleo kupitia CCM basi wakayatafute nje ya CCM”
Wakati sakala la Richmond lilipoibuka
miaka michache tu iliyopita, Chadema ilimfanya limsakama Lowassa kuwa ni mmoja
wa mafisadi wakubwa nchini. Lakini wakati chama hicho kinamkaribisha kuwa
mwanachama wao, kiligeuka na kusema hakuna mtu msafi nchini na kwamba hawawezi
kuacha kumpokea mwanasiasa mwenye mtaji mkubwa wa wafuasi kama Lowassa.
Wakati akiwa Waziri Mkuu, Lowassa
alisifika kama mchapakazi hodari na msimamiaji wa moja kwa moja wa shughuli za
serikali. Bado anaendelea kufahamika kwa jina la utani la ‘mzee wa maamuzi
magumu’.
Image caption Je unamfahamu Edward
Lowassa ni nani katika siasa za Tanzania ?
Moja ya mafanikio makubwa ya uwaziri
mkuu wake ni jitihada kubwa na mafanikio ya upatikanaji wa fedha za kujenga
chuo kikuu cha Dodoma. Chuo hiki kikuu cha umma kilichopo katikati ya Tanzania
kilianzishwa mwaka 2007.
Lowassa ni mashuhuri pia kwa kusimamia
mpango wa serikali uliofanikiwa wa ujenzi wa shule za kata ambazo uliiletea
Tanzania sifa kubwa kwa kutoa fursa ya watoto wengi kupata nafasi shuleni.
Mtoto wa Mzee Ngoyai Lowassa, ambaye
aliwahi kuwa mtumishi wa serikali ya kikoloni, Lowassa ameanza harakati zake za
kuwania urais tangu mwaka 1995 lakini inaarifiwa kwamba rais wa kwanza wa
Tanzania Mwl Julius Nyerere alimkatalia kushika nafasi hiyo. Wafuasi wa Lowassa
wamekuwa wakiyatupilia mbali madai hayo
Ulipofika uchaguzi wa mwaka 2005,
Lowassa hakutaka kuwania urais, lakini badala yake alimnadi rafiki yake wa siku
nyingi Rais wa sasa Jakaya Kikwete ambaye alipata ushindi wa kishindo wa zaidi
ya asilimia 80.na kennedyrutta
No comments:
Post a Comment