Maafisa wa polisi nchini Uganda
wameimarisha usalama katika maeneo mengi ya uma katika mji mkuu wa Kampala
kufuatia kukamatwa kwa washukiwa kadhaa wa makundi ya kigaidi na vilipuzi
.
Msemaji wa polisi mjusi kwamba
jaribio la kutekeleza mashambulizi limetibuliwa.
Awali ,ubalozi wa Marekani mjini
Kampala ulisema kuwa mamlaka ilitibua shambulizi la kigaidi lilokuwa limepangwa
na washukiwa wa kundi la Alshabaab.
Ubalozi wa Marekani umewataka raia
wake nchini Uganda kuendelea kukaa majumbani mwao.
Ubalozi huo tayari ulikuwa umeonya kuhusu
shambulizi la kulipiza kisasi dhidi ya maeneo ya Marekani na kundi la Alshabaab
ili kujibu shambulizi la angani la Marekani lililomuua kiongozi wa kundi hilo
mapema mwezi huu
No comments:
Post a Comment