Afrika Kusini: Oscar Pistorius aendelea kunufaika na dhamana

Mahakama yafuta tuhuma ya mauaji iliyokua inamkabili mwanariadha wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius, Septemba 11 mwaka 2014.
REUTERS/Siphiwe Sibeko
Na kennedyrutta
Kwa mujibu wa jaji wa mahakama ya mji wa Pretoria nchini
Afrika Kusini, Thokozile Masipa, Oscar Pistorius hana hatia ya kumuua
Reeva Steenkamp, mauaji ambayo yalitokea Februari 14 mwaka 2013. Hata hivo haimaanishi kuwa mwanariadha huyo hatohukumiwa.
Tangazo hilo limetolewa alhamisi wiki hii mchana : Jaji amebaini kwamba Oscar
|
Oscar Pistorius alimfyatulia risase mpenzi wake Reeva Steenkamp kupitia mlango huu.
REUTERS/Alexander Joe/Pool
|
|
hana
hatia ya mauaji. Kwa kutetea uamzi wake, hakimu huyo ameeleza kwamba
kuna tofauti kati ya kufyatua risase na kuwa na nia ya kuua. Je
mwanariadha huyo alikua na nia ya kuua mpenzi wake wakati alipofyatua
risase kwenye mlango
wa choo? Mwanariadha alikanusha mwenyewe na kusema
kwamba alifyatua risase kwenye mlango wa choo baada ya kusikia mtu
chooni akidhani kwamba ni mtu ambaye alikua amekuja kuhatarisha usalama
wake.
|
Mku
wa kikosi cha usalama nchini Arfika kusini, Pieter Baba, akitoa
ushahidi wake katika kesi ya Oscar Pistorius, mjini Pretoria, Machi 07
mwaka2014.
REUTERS/Schalk van Zuydam/Pool
|
|
Maswali
yote yako wazi, je alikua na dhamira ya kuua? Jaji, Thokozile Masipa,
amebaini hapana, kwa sababu ya mwenendo wake aliyouonesha muda mfupi
baada ya tukio hilo : alipigia sim vyombo vya usalama, wakati huo huo
alimpigia sim daktari ili aweze kuwasili eneo la tukio na kumfanyia
matibabu mpenzi wake huyo wa zamani ambaye alimfyatuliwa risase bila
kukusudia. Muda mchache uliyofuata, alibaini kwamba alikua
alijidanganya, hakua na nia ya kumuua. Jaji amesema kutokana na hali ya
uzuni aliyokua nayo, Oscar hangelikumbuka katika utetezi wake kusema
yote aliyoyafanya akijaribu kuokoa maisha ya Reeva Steenkamp.
Kutokana na utetezi wake, Oscar Pistorius hakupatikana na hatia
yakuua kwa kukusudia. Saa moja kabla, jaji alitupilia mbali hoja ya kuua
bila kukusudia iliyotolewa na mwendeshamashtaka dhidi ya Oscar.
Kinachosalia kwa sasa ni hukumu dhidi ya kuua bila kukusudia au
kuachiliwa huru. Lakini hata hivo, sheria ya jinai ya Afrika Kusini
haiweki wazi hukumu ya kosa la kuua bila kukusudia. Hukumu imetolewa,
lakini huenda Pistorius akapewa adhabu ya kufungwa jela au adhabu ya
kifungo jela ikiwa ni pamoja na faini. Jaji Thokozile Masipa amesema
adhabu hiyo itatolea Oktoba 13 mwaka 2014.
Jaji Masipa ametupilia mbali ombi la mashtaka la kutaka dhamana ya
Pistorius ibatilishwe, na kubaini kwamba upande wa mashtaka haukuonesha
umuhimu wowote wa kubatilisha dhamana hiyo na badala yake ameongeza muda
hadi pale uamzi wa adhabu urtakapochukuliwa.
Wakati hakimu alipotangaza kufuta tuhuma ya mauaji, Pistorius ameangua kiliyo, huku akitokwa na machozi mengi kizimbani.
|
Oscar Pistorius mwanariadha aneishi na ulemavu.
|
No comments:
Post a Comment