Saturday, 27 December 2014

Jumatano, 24 Disemba 2014 07:10 Uislamu na Mtindo wa Maisha(48) ukubwa wa hati ukubwa wa hati kuzisha hati Kichapishi Add new comment Uislamu na Mtindo wa Maisha(48) Hamjambo na karibuni kuwa nasi tena katika sehemu nyingine ya makala ya Uislamu na Mtindo wa Maisha. Makala yetu leo inaendelea kuzungumzia misingi ya jinsi ya kuamiliana na watoto kwa mujibu wa mtindo wa maisha wa Kiislamu. Wataalamu wa elimu nafsi wanasema kuwa, moja kati ya mahitaji muhimu ya mwanadamu baada ya mahitaji ya kimsingi ya kiumbe huyo kama maji na chakula, ni haja ya kupendwa. Kupendwa kuna umuhimu mkubwa sana kwa kadiri kwamba iwapo haja hiyo haitakidhiwa, basi suala hilo linaweza kuwa na taathira mbaya katika maisha ya mwanadamu. Haja ya kupendwa huwa kubwa zaidi katika nafsi ya mtoto na kukidhiwa kwake kwa njia sahihi ni nguzo na msingi muhimu wa malezi bora. Kumpenda mtoto humzidishia utulivu wa kiroho na kinafsi, hali ya kujiamini na kuwategemea na kuwaamini zaidi wazazi wake. Katika upande wa pili, kutoshibishwa haja hiyo ya kupendwa katika nafsi ya mtoto humuondolea utulivu na usalama wa kiroho na kinafsi, kumfanya asijiamini yeye na watu wengine, kujihisi hakiri na duni na pengine kumsababishia matatizo ya kimwili na kinafsi, utovu wa maadili na kutumbukia katika ufuska. Familia yenye mlingano katika mtindo wa maisha wa Kiislamu ni familia ambayo wanachama wake wanasifika kwa kuwa na uhusiano unaotawaliwa na upendo na mahaba baina yao. Viongozi wa dini yetu tukufu ya Uislamu pia wamefanya jitihada kubwa za kuwahimiza Waislamu kujenga uhusiano wao wa kifamilia kwa msingi wa upendo na mahaba baina yao. Imam Swadiq (as) ameeleza kuwa miongoni mwa mambo yanayoteremsha rehma za Mwenyezi Mungu kwa mja wake ni kumpenda sana mtoto. Anasema: “Mwenyezi Mungu humrehemu na kumteremshia rehma mtu anayempenda sana mwanaye”. Tumesema kuwa upendo na mahaba vimehimizwa sana kati ya watu wa familia. Hata hivyo tunasisitiza kuwa, uadilifu na insafu inapaswa kuzingatiwa na kuchungwa katika namna ya kuamiliana na watu ndani ya familia. Kwa mfano mahaba na upendo wa wazazi wawili kwa mtoto mmoja katika familia unapovuka mipaka ya uadilifu na insafu yumkini ukawa na taathira nyingi mbaya kwa watoto kama husuda, kujiona duni, kukata uhusiano na wazazi na kuwa na vinyongo kwa watoto wengine. Vilevile kuamiliana kibaguzi na watoto yumkini kukahatarisha msingi wa familia katika siku za usoni. Kwa kuzingatia hayo Mtume Muhammad (saw) alipomuona bwana mmoja akimbusu mmoja kati ya watoto wake na kumuacha mwingine alilalamika na kumwambia: Kwa nini huamiliani nao kwa usawa? Mtukufu Mtume pia amewaambia Waislamu kwamba: “Amilianeni na watoto wenu kwa uadilifu kama mnavyopenda kufanyiwa wema na uadilifu”. Taasisi ya familia inapaswa kuwa anga iliyojaa upendo na mahaba. Anga ya utulivu, upendo na mahaba ndani ya familia na mwenendo mzuri wa wazazi kwa watoto huwa na shifaa na tiba ya kinafsi kwa watoto na huwatayarishia mazingira mazuri ya kustawi katika nyanya mbalimbali. Aina ya uhusiano wa wazazi na watoto wao ndani ya familia huwa msingi wa mahusiano yao ya baadaye na watu wengine. Imam Muhammad Ghazali anasema katika kitabu cha Kemia ya Saada kwamba: Elewa kwamba, mtoto ni amana katika mikono ya baba na mama, na nafsi yake safi ni mithili ya johari yenye thamani kubwa. Ni kama nta inayokubali umbo na sura tofauti, na mithili ya ardhi safi ambayo kila kinachopandwa humo kinaota na kumea. Kama utapanda mbegu ya kheri katika ardhi hiyo itamfikisha katika saada na ufanisi wa dunia na akhera, na baba, mama na mwalimu watashirikiana na mtoto huyo katika thawabu zake; na kinyume chake, mtoto huyo hukumbwa na masaibu na wazazi na mwalimu hushirikiana naye pia katika hayo”, mwisho wa kunukuu. Miongoni mwa mambo muhimu kuhusu suala la kuwapenda watoto ni kwamba tusitosheke na kuwapenda katika nyoyo zetu tu, kwani upendo na mahaba huwa na taathira pale vinapodhihirishwa na kumuonesha mtoto kwamba anapendwa. Imam Ali bin Abi Twalib (as) alidhihirisha upendo na mahaba yake kwa mwanaye, Hassan bin Ali (as), katika barua aliyomwandikia akisema: “Nakutambua kuwa wewe ni sehemu yangu mimi bali wewe ni mimi mzima kwa kadiri kwamba kinachokusibu wewe huwa kama kimenisibu mimi na kana kwamba mauti yakikufika wewe ni sawa na kunifika mimi. Hivyo basi mambo yako yanaishughulisha nafsi yangu kama ninavyoshughulishwa na yangu mwenyewe na kwa msingi huo nakuandikia barua hii ili nipate kudhihirisha upendo na mahaba yangu kwako..”. Kuonesha na kudhihirisha upendo na mahaba ni miongoni mwa misingi muhimu ya uhusiano wa wazazi na watoto wao. Hali zetu za kiroho hutusaidia sana katika kuchukua maamuzi na kutoa hukumu na maoni. Vilevile wazazi wanaodhihirisha upendo na mahaba kwa watoto huzidisha hali ya upendo na mahaba baina yao wenyewe na matokeo yake ni kuimarisha uhusiano wa watoto na wazazi wao. Wataalamu wa elimu nafsi wanasema kuwa, utafiti uliofanywa kuhusu upotofu na utovu wa maadili wa watoto umebaini kuwa, kuna sababu nyingi za jambo hilo ikiwa ni pamoja na ukosefu wa mahusiano mazuri na yenye upendo na mahaba ya wazazi kwa watoto wao. Mafundisho ya Uislamu yamehimiza sana juu ya udharura wa kudhihirisha hisia za ndani ya nafsi. Mazungumzo yaliyojaa hisi za upendo na mahaba kwa watoto, kumtazama mtoto kwa jicho na upendo, mahusiano yasiyo ya maneno na watoto kama kumbusu, kumpakata na kumpapasa kichwani kulingana na umri wa mtoto, ni miongoni mwa vielelezo vya kudhihirisha hisi za upendo na mahaba kwa mtoto wako. Mtume Muhammad (saw) anasema kuhusu suala hilo kwamba: Mtu anayembusu mtoto wake, Mwenyezi Mungu humwandikia amali njema, na mtu anayemfurahisha mtoto wake M, Mungu atamfurahisha Siku ya Kiyama". (Usulul Kafi: 6-49) Miongoni mwa misingi muhimu ya uhusiano wa wazazi na watoto ni kuwaruhusu kueleza mitazamo, hisia na maamuzi yao kwa uhuru. Suala hilo lina maana kwamba, tutakuwa tumempa mtoto haki ya kukosea isipokuwa katika masuala ambayo makosa kama hayo ni hatari kwake yeye na kwa watu wengine. Kabla ya jambo lolote, wazazi wawili wanapaswa kuwa wasikilizaji wazuri ili waweze kuwa wasaidizi na waelekezaji bora wa watoto wao. Watoto wana haja ya kuhisi kwamba, wanapendwa na kukubaliwa na wazazi wao, japo wakati mwingine wanakosea na kutumbukia katika makosa. Kabla ya watoto kuwa tayari kusikiliza maneno ya mzazi, wanapaswa kwanza kuhisi kwamba maneno yao yanasikilizwa na wazazi, na kabla ya kueleza fikra, hisia na matakwa yao, kwanza wanapaswa kufikia natija kwamba wazazi wao wanawaelewa na kuwathamini. Dakta Ghulam Ali Afruz ambaye ni mtaalamu wa saikolojia wa Iran anasema: Mtoto ana haki ya kepata upendo, utanashati na hisia za kukubalika ndani ya taasisi ya familia. Anaendelea kwa kusema: Mtume Muhammad (saw) amesema, katika miaka saba ya kwanza ya uhai wake, mtoto huwa mwenye kupendwa, na kipindi cha miaka saba ya pili huwa tayari kufundishwa na katika saba la tatu huwa mshauri. Kipindi cha miaka saba ya awali ndicho kipindi cha kuweka misingi imara ya shakhsia ya mtoto. Kwa kawaida watoto hupenda kupitisha kipindi hicho kwa utanashati, upendo na katika anga ya uhusiano wenye vuguvugu na mahaba ya wazazi. Vilevile watoto wana haki ya kuheshimiwa, na hupendelea kuthaminiwa na kuenziwa na watu wengine. Kwa msingi huo, anamalizia Dakta Ghulam Ali, miongoni mwa nyadhifa muhimu na majukumu makubwa ya baba na mama ni kuwakirimu, kuwathamini na kuwaheshimu watoto wao.


Hamjambo na karibuni kuwa nasi tena katika sehemu nyingine ya makala ya Uislamu na Mtindo wa Maisha. Makala yetu leo inaendelea kuzungumzia misingi ya jinsi ya kuamiliana na watoto kwa mujibu wa mtindo wa maisha wa Kiislamu.
Wataalamu wa elimu nafsi wanasema kuwa, moja kati ya mahitaji muhimu ya mwanadamu baada ya mahitaji ya kimsingi ya kiumbe huyo kama maji na chakula, ni haja ya kupendwa. Kupendwa kuna umuhimu mkubwa sana kwa kadiri kwamba iwapo haja hiyo haitakidhiwa, basi suala hilo linaweza kuwa na taathira mbaya katika maisha ya mwanadamu. Haja ya kupendwa huwa kubwa zaidi katika nafsi ya mtoto na kukidhiwa kwake kwa njia sahihi ni nguzo na msingi muhimu wa malezi bora. Kumpenda mtoto humzidishia utulivu wa kiroho na kinafsi, hali ya kujiamini na kuwategemea na kuwaamini zaidi wazazi wake.Jumatano, 24 Disemba 2014 07:10 Uislamu na Mtindo wa Maisha(48) ukubwa wa hati ukubwa wa hati kuzisha hati Kichapishi Add new comment Uislamu na Mtindo wa Maisha(48) Hamjambo na karibuni kuwa nasi tena katika sehemu nyingine ya makala ya Uislamu na Mtindo wa Maisha. Makala yetu leoi

Kiongozi wa Al-Shabaab akamatwa





Kundi la wapiganaji wa Al shabaab
Maafisa nchini Somali wanasema kuwa kiongozi mkuu wa kundi la wapiganaji wa Alshabaab amekamatwa karibu na mji mmoja karibu na mpaka wa Kenya na Somali